Ubora wa huduma kwa wazee: Utafiti kwa wataalamu wa afya na matunzo na wasimamizi

Caution: JavaScript execution is disabled in your browser or for this website. You may not be able to answer all questions in this survey. Please, verify your browser parameters.

Utangulizi na ridhaa

Karibu, na asante kwa kuchangia katika utafiti huu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu huduma bora za afya kwa watu wazee.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaandaa Viwango vya Kimataifa vya Ubora wa Huduma kwa Wazee. Utafiti huu unalenga kuelewa mambo ambayo wataalamu na watoa huduma za afya na matunzo, wakiwemo wasimamizi wa programu, wanaona kuwa muhimu katika kutoa huduma bora kwa wazee, pamoja na aina ya msaada unaohitajika ili kufanikisha hilo.

Tunapozungumzia ubora wa huduma, tunamaanisha huduma zenye matokeo mazuri, salama, zinazomzingatia mtu, zinazotolewa kwa wakati, zenye usawa, zilizounganishwa, na zinazotumia rasilimali ipasavyo. Tungependa kujifunza kutokana na uzoefu wako kuhusu mambo yanayofanya kazi vizuri, changamoto unazokabiliana nazo, na maboresho yanayoweza kufanywa ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wazee. Maoni yako yatasaidia katika kuandaa viwango vya kimataifa vya siku zijazo vya huduma bora kwa wazee. 

Nani anaweza kushiriki?

Unaweza kushiriki ikiwa: wewe ni mtaalamu wa afya au matunzo, au msimamizi wa programu ya afya, unayetoa, kusimamia au kupanga huduma za afya na/au matunzo kwa watu wazee (wenye umri wa miaka 60 au zaidi); na unaweza kuelewa maelezo ya utafiti na kujaza dodoso katika mojawapo ya lugha zinazopatikana.

Kujaza utafiti kunachukua takribani dakika 30–35. 

Maswali mengi yanauliza mambo ambayo yanapaswa kuwepo ili kutoa huduma bora kwa wazee. Baadhi ya maswali yanahusu uzoefu wako wa sasa au mazingira unamofanya kazi. Maswali yenye alama ya nyota (*) ni ya lazima na yanapaswa kujibiwa ili kuendelea. Tafadhali jibu maswali mengine yote kwa ukamilifu na usahihi kadri uwezavyo. Ukiacha mojawapo bila jibu, ujumbe wa kukukumbusha utaonekana unapobofya “Inayofuata” au “Wasilisha”; hata hivyo, unaweza kuendelea bila kujibu. Majibu yako katika sehemu zote za utafiti ni muhimu kwa kuelewa mahitaji, uzoefu na maoni ya wataalamu wa afya na matunzo katika mazingira tofauti. 

Ushiriki wako

Ushiriki wako ni wa hiari. Majibu yako hayatakuwa na utambulisho wako na yatatunzwa kwa siri. Hakuna majibu sahihi au yasiyo sahihi. Unaweza kuacha utafiti wakati wowote kabla ya kuwasilisha majibu yako.

Kwa kuwa hatukusanyi taarifa zinazoweza kukutambulisha, hatutaweza kukupata au kufuta majibu yako mara baada ya kuwasilisha majibu yako ya utafiti huu. 
Kwa kuwasilisha utafiti, unathibitisha kuwa umesoma na kuelewa maelezo hapo juu na unakubali kwa hiari kushiriki, pamoja na kukubali majibu yako yakusanywe na kuchakatwa kwa madhumuni yaliyoelezwa. 

Ikiwa una maswali, tafadhali wasiliana na Dkt. Yuka Sumi, Afisa wa Afya, Shirika la Afya Duniani, kwa barua pepe: sumiy@who.int. 

Asante sana kwa mchango wako.

There are 93 questions in this survey.